Mashine mbalimbali za Norwood za kuchana mbao

Ni mashine ya kuchana mbao inayouzwa bei nzuri na imara yenye kutengeneza faida kwa Biashara yako

 • Kuwa kiongozi kwenye jamii yako.
 • Zalisha mbao zenye ubora na kujenga biashara yenye faida.
 • Hifadhi misitu ya Africa kwa mpango endelevu na kwa faida ya vizazi vijavyo.

Unaweza kufanikisha haya yote, na zaidi, kwa kumiliki mashine ya Norwood band sawmill

Kwa jinsi gani? Soma yafuatayo.

 1. Kuhamasisha kuchana magogo katika eneo lako, inapelekea kutengeneza ajira na kukuza uchumi katika jamii yako.
 2. Unapo chana magogo na kutengeneza mbao na inakuwa umeongeza thamani ya misitu, ambapo unaweza kuuza mbao zako kwa wajenzi wa nyumba, mafundi seremela na wachonga vinyago nk.
  Soma maelezo zaidi hapo chini, ujue kwanini mashine ya Norwood sawmills ni chaguo sahihi kwako.
 3. Kwa ujumla uvunaji wa miti hupunguza uharibifu na taka za makampuni ya mbao za megaChinese. Norwood bandmills hutumia tekinolojia ya thin-kerf - hii ina maana msumeno mwembamba sana wenye kuchana na unatoa taka chache pia hutoa mbao nyingi za kuuza.

Kwa nini Norwood Sawmills ni chaguo sahihi kwako? ni kwa sababu chache zifuatazo...

Msunobari, mkangazi/mbambakofi, Loliondo, Mgunga, Mpingo nk ni miti migumu(miti chuma) ya Africa ambayo ni miti migumu duniani. Kazi ya kuchana mbao kwa miti ya Africa ni kazi kubwa na ngumu Hivyo basi Norwood Sawmills imetengenezwa mahusisi kuondoa changamoto za uchanaji miti migumu ya Africa.

Norwood, ni miongoni mwa kampuni kubwa za sawmills imara duniani, iliyoanzishwa miaka 25 iliyopita.

Kuna sababu kuu zinazofanya Norwood sawmills kuwa chaguo sahihi kwako.

Wazo jipya
Ina zaidi ya hati miliki 50, ambazo ni zaidi ya kampuni zote zingine za sawmill ulimwenguni.
Uzalishaji
Technologia ya Norwood huokoa muda na kubadili gogo kuwa mbao. Kwa kupunguza nguvu za kazi, zina mzunguko wenye kasi na uwezo mkubwa. Mashine za Norwood sawmills zina uzalishaji mkubwa na hutengeneza faida kuliko kampuni zingine za sawmill.
Madhubuti
Kila mashine ya Norwood sawmills imetengenezwa kwa uimara mkubwa na inaweza kuchana mbao usiku na mchana mfululizo bila kufanyiwa marekebisho yoyote. Norwood sawmills ni rahisi kutumia, kukagua na ni za uhakika.
Ufanisi
Norwood sawmills zina ufanisi mkubwa na huongeza thamani ya ubao na mbao zako. Je unahitaji mbao zenye mvuto na zilizonyooka na zenye mkato mwembamba? Mashine za Norwood sawmill zimetengenezwa kutoa huduma hizo.
Bei nafuu
Norwood sawmills ni za bei nafuu. Ukweli ni kwamba! ukilinganisha kifaa kwa kifaa, utengenezaji na ubora wa ufungaji, Norwood sawmills ni bora na ni madhubuti kuliko mashine nyingine za kuchana mbao zilizopo sokoni.
Rahisi kusafirisha
Mashine za Norwood hupakiwa kwenye kifurushi kimoja kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji na kukufanya kuokoa maelfu ya shilingi kwenye gharama za usafirishaji, Ahsante kwa mfumo huu wa upakiaji kwa kusafirisha mashine hii kwa pamoja. Faida nyingine pale mmiliki anapo unganisha mashine yeye mwenyewe inamfanya apate uzoefu wa kujua mashine vizuri nje na ndani na hata kumrahisishia katika marekebisho na kutengeneza faida ya uhakika.

Fahamu mashine ya Norwood LumberMate LM29 Sawmill - Mashine Madhubuti ya kuchana mbao barani Africa.

 1. Ina uwezo wa kuchana miti/magogo yenye upana sentimita 74-milaini na migumu.
 2. Hutoa mbao zenye upana wa hadi sentimita 56.
 3. Ina uwezo wa kuchana magogo yenye urefu wowote- Mfano, Mashine ya Lumber Mate LM29 Mills huchana ubao wenye urefu wa mita 3.8, lakini unaweza kuongeza kadri utakavyo hadi urefu wa mita 1.2 unaweza kupanua eneo la kuweka gogo pale unapohitaji kuchana miti mirefu.
 4. Uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea- Inauwezo wa kupakia magogo na kuyaongoza kwenye eneo la kuchana kirahisi na kukata bila umeme.
  Hakuna ulainishwaji wa mafuta unao hitajika wala kutegemea vifaa vya umeme kujiendesha.
 5. Kuokoa muda na Kuongeza uzalishaji;- Mashine hizi zina msumeno ambao hujiseti wenyewe na kuondoa haja ya kufunga na kufungua wakati wa kuchana magogo.
 6. Zina beringi za kuongoza msumeno nazina gurudumu, hivyo hurahisisha haja ya matengenezo.
 7. Huja na clamp zenye skruu za kufungia magogo na hugeuza gogo kwenye eneo lake.
 8. Kuna viambatanisho vifuatavyo:
  a. Log deck extensions (1.2m/each) (Reki ya kupanua mahali pa kuweka gogo (1.2m/@)
  b. Trailer system with sub-frame and support legs (Tela yenye fremu na miguu ya kujitegemea)
  c. Log loading ramps and winch (Mkono wa kunyanyulia magogo)
  d. Cam log clamp (clamp ya kubania magogo)
Modeli
Nguvu
Bei*
LumberMate LM29 (zinafungashwa na vipeperushi venye maelekezo)
Electric (7,5Kw 380 v)
Tsh 11,645,922.73
LumberMate LM29 (zinafungashwa na vipeperushi venye maelekezo)
Petrol (16hp V-Twin Vanguard)
Tsh 13,562,947.05
LumberMate LM29 (zinafungashwa na tela)
Petrol (16hp V-Twin Vanguard)
Tsh 18,435,383.85
*Bei ni kwa Tsh Norwood Sawmills kituo cha usambazaji, Roodepoort, Afrika Kusini na bei sio pamoja kodi. Bei itaongezeka/kupungua kutegemea vigezo kama vile gharama za kutuma na viwango vya kubadilishana fedha.

Kwa msaada sawmill zenye ukubwa zaidi!

LumberPro HD36 inaukubwa wa 70cm katika mduara, kwa ukubwa huo unaweza kukata magogo hadi urefu wa 91 katika mduara, wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.

Norwood Sawmills imefika Afrika ... Na Sisi tupo kukuletea bidhaa yetu!!

Norwood huhifadhi bidhaa zake kwenye ghala tatu za uhakika kwa ajili ya usambazaji Kaskazini mwa Africa, Africa Kusini Zambia na Uganda. Kwa uwepo wa sehemu hizi za maghala, Norwood inaweza kusambaza bidhaa zake kwa haraka zaidi katika nchi za jirani. Pia wataalamu wa Norwood wako katika sehemu zilizotajwa hapo juu kwa msaada zaidi wasiliana nasi.

Kupata majibu ya maswali yako kuhusu bidhaa za Norwood Sawmills, kupata garama za bidhaa, au kununua bidhaa wasiliana na Norwood Sawmills Africa kwa barua pepe au simu zilizopo kwenye tovuti yetu. Tunategemea kukuhudumia katika mahitaji yako ya viwanda vya uchaanaji wa mbao.

Tembelea tovuti yetu www.NorwoodSawmills.com.